MUZAMILU YASSINI KUIKOSA NJE SIMBA DHIDI YA STAND UNITED JUMATANO
SIMBA SC iko hatarini kumkosa kiungo wake tegemeo, Muzamil Yassin katika
mchezo wake ujao wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya Stand
United Jumatano.
Simba SC watacheza mechi ya pili mfululizo Uwanja wa Kambarage,
Shinyanga Jumatano wakati timu yao itakapomenyana na Stand, ikitoka
kushinda 3-0 dhidi ya Mwadui juzi.
Na Daktari wa Simba SC, Yassin Gembe amesema kwamba Muzamil aliumia kifundo cha mguu juzi katika mchezo na Mwadui.
Muzamil Yassin (kushoto) aliumia kifundo cha mguu katika mchezo dhidi ya Mwadui, lakini leo anatarajiwa kufanya mazoezi
Lakini Gembe alisema kwamba maumivu ya Muzamil aliyesajiliwa Simba SC
msimu huu kutoka Mtibwa Sugar ya Morogoro hayatarajiwi kuwa makali ya
kumuweka nje muda mrefu.
“Aliumia enka, lakini hatutarajii yawe maumivu makali sana. Nadhani
Jumatatu ataweza kufanya mazoezi baada ya mapumziko ya saa 24,”alisema.
Gembe alisema majeruhi ambaye ataendelea kuwa nje ya programu za timu ni
mshambuliaji Muivory Coast, Frederick Blagon ambaye amebaki Dar es
Salaam kwa matibabu.
Gembe alisema kwamba Blagnon baada ya wiki moja ya mapumziko, atahitaji
tena japo siku tatu za kufanya mazoezi ili kuwa fiti - maana yake
atakuwa a jumla ya wiki zisizopungua mbili za kuwa nje tangu aumie wiki
iliyopita kwenye mechi na Toto Africans Simba ikishinda 3-0 Uwanja wa
Uhuru, Dar es Salaam.
Comments
Post a Comment