Pogba na De Gea waomba msamaha kwa sare dhidi ya burnley
Kama ilivyo kwa mashabiki wengi wa Manchester United, Paul Pogba na
David De Gea wameonesha kusikitishwa na mfululizo wa matokeo
yasiyoridhisha ya Manchester United hasa katika mchezo wa jana dhidi ya
Burnley uliochezwa Old Trafford na kumalizika kwa suluhu, huku United
wakifanya mashambulizi mengi yasiyozaa matunda.
Hali hiyo imesababisha United kuweka rekodi mpya katika historia ya klabu hiyo kwa kuanza msimu vibaya kuliko wakati wowote ule.
Kipa wa Burnley Tom Heaton ndiyo alikuwa nyota wa mchezo baada ya kuzuia michomo mingi, huku Zlatan akishindwa kufunga kwenye mchezo wa sita mfululizo na kuweka rekodi ya kucheza michezomingi zaidi bila ya kufunga kwenye historia ya maisha yake ya soka.
Tukiolingine ni kitendo cha kocha wa klabu hiyo Jose Mourinho kuondolewa kwenye benchi la ufundi na kupelekwa kukaa kwenye majukwaa ya mashabiki baada ya kutoa lugha isiyoridhisha kwa refarii.
Baada ya matukio yote haya, David De Gea na Paul Pogba kupitia Instagram zao wameamua kuja na ujumbe chanya kuwafariji wapenzi wao.
De Gea ameandika hivi kwenye Instagram yake “Unbelievable how the victory escaped… But the team did a great effort, that’s the way Your support, always fantastic!!”.
Pogba akaandika: “Football results can be cruel but that’s one more reason to keep working and loving it”

Comments
Post a Comment