Polisi yasema imepata faida mil 690 kutokana na makosa mbali mbali
POLISI Kanda Maalumu ya Dar es Salaam kupitia kikosi chake cha
Usalama Barabarani kimekusanya zaidi ya Sh milioni 690, kupitia tozo za
makosa ya usalama barabarani.
Kamanda wa Polisi wa Kanda hiyo, Simon Sirro alisema faini hizo ni kuanzia Oktoba 18 hadi 25 mwaka huu.
Kwa mujibu wa Sirro, idadi ya magari yaliyokamatwa yalikuwa ni
20,833, idadi ya pikipiki zilizokamatwa zilikuwa ni 2,171 na daladala
zilizokamatwa zilikuwa ni 8,435.
Alisema magari mengine ambayo ni binafsi na malori yaliyokamatwa
yalikuwa ni 12,398 na waendesha bodaboda waliofikishwa mahakamani kwa
makosa ya kutovaa helmeti na kupakia mshikaki walikuwa 96.
Kamanda Sirro alisema jumla ya makosa yaliyokamatwa ni 23,004 na
fedha zilizotozwa ni 690,120,000 na hivyo kuiingizia serikali mapato.
Alitoa wito kwa wananchi wote kuzingatia sheria za usalama barabarani
ili kuondokana na ajali zisizo za lazima zinazosababisha majeruhi na
wakati mwingine vifo kwa watu wasio na hatia.
“Kila mmoja akizingatia sheria ya usalama barabarani ajali
zitapungua… wenye pikipiki wahakikishe wanavaa helmeti na waache kupakia
mshikaki, tukifanya hivyo ajali zitapungua,” alisema
Comments
Post a Comment