Rais Jacob Zuma asinzia bungeni wakati wakusoma bajeti ya nchi
Macho ya wengi nchini Afrika Kusini jana yalikuwa kwenye Waziri wa Fedha Pravin Gordhan ambaye alikuwa akihutubu bungeni.
Uchumi wa Afrika Kusini umekuwa ukikabiliwa na matatizo na kumekuwa na maswali mengi kuhusu ufadhili wa elimu.
Wanafunzi katika vyuo vikuu vingi wamekuwa wakiandamana na kuzua vurugu kulalamikia viwango vya karo.
Bw
Gordhan mwenyewe amejipata kwenye mzozo wa kisiasa na hivyo basi
taarifa yake ya bajeti ya muda ilisubiriwa kwa hamu na ghamu.
Lakini
asubuhi hii, habari zimeanza kuenea mtandaoni kwamba Rais Jacob Zuma
huenda alisinzia (au kupumzisha macho kama wasemavyo Kenya) wakati wa
hotuba ndefu ya waziri huyo.
Comments
Post a Comment