RAIS MAGUFULI KUFUNGUA BARA BARA HUKO KENYA
Rais wa Tanzania John Magufuli anatarajiwa kuanza ziara yake ya
Barabara hiyo, ambayo inaunganisha maeneo mbalimbali ya jiji la Nairobi kwa barabara za juu na chini, ni moja kati ya miradi mbalimbali ya ujenzi wa barabara ambayo imekuwa ikitekelezwa na serikali ya Kenya kupunguza msongamano wa magari katika jiji hilo kuu.
Rais Magufuli anatarajiwa kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta Jijini Nairobi majira ya saa nne asubuhi na baadaye kupokelewa rasmi na mwenyeji wake Rais Kenyatta katika Ikulu ya Nairobi ambako viongozi hao watafanya mazungumzo rasmi.
"Katika ziara hii Rais Magufuli anatarajiwa kutembelea kiwanda cha maziwa cha Eldoville kilichopo Karen Jijini Nairobi, na pia anatarajiwa kuzindua barabara mchepuko ya Southern By-pass iliyopo Jijini Nairobi," taarifa kutoka ikulu ya Tanzania imesema.
Comments
Post a Comment