Tanzania Yapata Mkopo Wenye Masharti Nafuu Wa Zaidi Ya Shilingi Bilioni 300 Kutoka Benki Ya Maendeleo Ya Afrika (Afdb) Na Serikali Ya Korea

Image result for picha za pesa za tanzania

 Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango (kulia) akitia saini makubaliano ya uteuzi wa mradi utakao fadhiliwa kwa pamoja kati ya Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) na Serikali ya
Korea, wenye thamani ya dola Milioni 50 za Marekani sawa na zaidi ya shilingi Bilioni 100.18 zitakazotumika kujenga njia ya usafirishaji umeme kwanjia ya gridi ya Taifa, yenye msongo wa kV 400 katika ukanda wa kaskazini Magharibi itakayoanzia mkoani Mbeya, Nyakanazi hadi Mkoani Kigoma.

TANZANIA, Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) na Korea ya Kusini zimetiliana saini makubaliano ya pamoja kutekeleza mradi wa ujenzi wa njia ya umeme gridi ya Kaskazini Magharibi inayoanzia mkoani Mbeya, Nyakanazi hadi Kigoma, yenye msongo wa kV 400 mbapo Serikali ya Korea imeahidi kutoa Dola za Marekani milioni 50 sawa na zaidi ya shilingi Bilioni 100.18, kwa ajili ya kugharamia mradi huo.

Hali kadhalika, Tanzania na Benki ya Exim ya Korea, zimesaini  Mkataba wa mkopo wenye masharti nafuu wa Dola za marekani milioni 90.092 sawa na zaidi ya shilingi Bilioni 194 za Tanzania, kwa ajili ya mradi wa Upanuzi wa Miundombinu ya mfumo wa maji taka Jijini Dar es salaam.

Comments