TRUMP aonyesha jeuli ya pesa azindua hotel yake kalibu na white house huko marekani
Mgombea urais wa
chama cha Republican nchini Marekani Donald Trump ataachana na kampeni
kwa muda na kufungua jumba lake la hoteli ya Trump International lililo
hatua chache kutoka ikulu ya White House.
Bw Trump atakata utepe
katika hafla hiyo ya kuzindua jumba hilo Washington DC kisha arejelee
kampeni katika jimbo la Carolina Kaskazini.
Mpinzani wake Hillary
Clinton atatumia siku yake hii, ya kuadhimisha miaka 69 tangu kuzaliwa
kwake, akifanya kampeni jimbo muhimu la Florida.
Bw Trump ana
habari njema kiasi kwamba kura ya maoni ya Bloomberg Politics inasema
anaongoza kwa asilimia mbili katika jimbo hilo.
Comments
Post a Comment