UBIGWA WA KOMBE LA SHIRIKISHO WANUKIA TP MAZEMBE


Image result for picha tp mazembe

Mechi ya kwanza ya Fainali ya Mashindano ya CAF ya Kombe la Shirikisho ilichezwa Jana Usiku huko Bilda Nchini Algeria ndani ya Stade Mustapha Tchaker nabWenyeji MO Bejaia kutoka Sare 1-1 na TP Mazembe ya Congo DR.

Bao za Mechi hiyo zilufungwa kila kipindi na Jonathan Bolingi ndie alieipa TP Mazembe Bao Dakika ya 43 na MO Bejaia kusawazisha Dakika ya 66 Mfungaji akiwa Yaya Faouzi.
Hii ni mara ya pili kwa Timu hizi kukutana kwenye Mashindano haya Mwaka huu kwani zilikuwa Kundi moja ambalo pia Yangavya Tanzania ilikuwemo na TP Mazembe ndio waliibuka Vinara na MO kushika Nafasi ya Pili huku zikitoka 0-0 huko Algeria na TP Mazembe kushinda 1-0 huko Lubumbashi kwa Bao la Dakika ya 62 la Mzambia Rainford Kalaba.
Mechi ya Marudiano ya Fainali hii itachezwa huko Stade TP Mazembe Mjini Lubumbashi Nchini Congo DR hapo Novemba 6.
VIKOSI:
MO Bejaia: Rahmani, Ferhat (Belkacemi 60), Rahal, Yaya, Khadir, Sidibe, Athmani, Betorangal, Benmelouka, Salhi, Bouali.
Mazembe: Sylvain Gbohouo - Issama Mpeko, Salif Coulibaly, Roger Assale, Merveille Bope, Nathan Sinkala, Jona.

Comments

Popular Posts