UMOJA WA MATAIFA WAJA NA NENO ZITO JUU YA KENYA KUFUTA HUKUMU YA KIFO
Siku
chache baada ya Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya kubatilisha hukumu ya Kifo
na kuwa kifungo cha maisha jela, Umoja wa Mataifa umepongeza
maamuzi ya
Kenya juu ya kufuta adhabu ya kifo kwa maelfu ya watu waliokuwa
wakisubiri kutekelezwa hukumu hiyo dhidi yao.
Kwa
mujibu wa msemaji wa wa idara ya Haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa
Ravina Shamdasani, amesema hatua hiyo ya serikali ya Kenya ni ya
kupongezwa, yenye kutia matumaini na inayofaa kufuatwa na nchi nyingine.
Ravina amesema anaamini kuwa serikali ya Kenya itafanya mikakati ili
kuhakikisha kuwa hukumu hiyo inafutwa kabisa kwa misingi ya sheria na
katiba.
Rais Uhuru Kenyatta, Jumatatu iliyopita
alibadili hukumu zote za kifo katika nchi hiyo ya Afrika Mashariki na
kuzifanya kuwa kifungo cha maisha jela. Hatua hiyo imewaondolea adhabu
ya kifo wafungwa 2,747 katika nchi hiyo ambayo haijamyonga mfungwa
yeyote aliyehukumiwa kifo kwa kipindi cha miaka 30 mpaka sasa.
Kupunguzwa
adhabu ya kifo kwa idadi kubwa ya wafungwa kulifanyika mara ya mwisho
nchini Kenya mwaka 2009 wakati wa utawala wa Rais mtaafu Mwai Kibaki.
Ripoti zimearifu kuwa, hukumu ya kifo ilitekelezwa mara ya mwisho nchini
Kenya mwaka 1987.
Comments
Post a Comment