VIGOGO KIKAANGONI KWA UPOTEVU WA SHILINGI MILIONI 410

Watumishi watano wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbozi mkoani Songwe waliohamishwa na wengine kustaafu wanatakiwa kurejeshwa ili kutoa maelezo ya matumizi ya Sh410 milioni zilizopotea katika mazingira tata.

Vigogo wanaotakiwa kurudi Mbozi baada ya kuhamishwa 2012/13 ni waliokuwa wakishikilia nyadhifa za mkurugenzi mtendaji, mweka hazina, ofisa elimu sekondari, ofisa mipango na mganga mkuu wa wilaya.

Taarifa hiyo, ipo kwenye mapendekezo ya tume iliyoundwa na Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Luteni Mstaafu Chiku Galawa kuchunguza upotevu wa fedha hizo.

Comments