Wakamatwa kwa mauaji ya vikongwe
MKUU wa Wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga, Fadhili Nkurlu, amesema watu 22 wanashikiliwa na Polisi wilayani hapa kwa tuhuma za kuhusika na mauaji ya vikongwe.
Alisema, idadi hiyo ilijulikana baada ya msako uliofanywa na Kamati ya Ulinzi na Usalama kwa kushirikiana na kikosi maalumu kutoka Wizara ya Mambo ya Ndani.
Alisema hayo katika kikao cha kawaida cha Baraza la Madiwani cha Halmashauri ya Msalala na kuongeza kuwa, chanzo cha mauaji hayo ni ramli chonganishi zilizokuwa zikifanywa na waganga wa kienyeji katika maeneo mbalimbali wilayani humo. Nkurlu alisema kuwa wapiga ramli 11 wanashikiliwa na Polisi kwa kusababisha vifo katika maeneo mbalimbali
Comments
Post a Comment