YANGA YAWEKA REKODI NYINGINE KALI
YANGA siku tano bao 10! ndivyo ilivyotokea jana baada ya mabingwa hao
watetezi wa Ligi Kuu kushinda mabao 4-0 dhidi ya JKT Ruvu na hivyo kuwa
na mabao 10 ndani ya siku tano baada ya kuifunga Kagera Sugar mabao 6-2
Jumamosi iliyopita.
Kwa wastani wa kila mechi goli 5 kwa mechi mbili walizo cheza mpka sasa Ushindi huo uliopatikana kwenye uwanja wa Uhuru Dar es Salaam
umeifanya Yanga kuendelea kushika nafasi ya pili kwenye msimamo ikiwa na
pointi 24, tofauti ya pointi tano na vinara wa ligi hiyo, Simba. Katika
mechi hiyo ya kiporo, Yanga ilitawala katika vipindi vyote vya mchezo.
Obrey Chirwa nyota yake iliendelea kung’ara jana baada ya kufunga bao la kuongoza katika dakika ya tano ya mchezo huo.
Alifunga bao hilo kwa shuti baada ya kuunganisha mpira wa Simon
Msuva. Mshambuliaji huyo sasa amefikisha mabao matano. Amisi Tambwe
aliifungia Yanga bao la pili katika dakika ya 63.
Alifunga bao hilo baada ya kuukokota mpira nje ya 18 huku mabeki ya
Ruvu wakimsindikiza kabla ya kuachia fataki lililojaa wavuni. Dakika ya
82, Msuva alifunga bao la tatu kwa kazi nzuri ya Tambwe aliyempigia
pande murua.
Tambwe aliibua tena shangwe kwa mashabiki wa timu hiyo baada ya
kufunga bao la nne katika dakika ya 90 baada ya kumzidi ujanja mlinzi wa
Ruvu, Michael Aidan aliyekuwa akirudisha mpira kwa kipa wake na Tambwe
kuuwahi na kuujaza wavuni.
Comments
Post a Comment