AFISA MTENDAJI AHUKUMIA JELA KWA KUMKATISHIA MASOMIO MTOTO WAKE
OFISA Mtendaji wa Kijiji cha Mpanji, Kata ya Mpanji, wilayani
Tunduru, mkoani Ruvuma, Jimmy Bandawe na wakazi wanne wa kijiji hicho,
wamehukumiwa kwenda jela miezi miwili au kulipa faini ya Sh
200,000 kwa
kosa la kukatisha masomo watoto wao.
Mbali na Ofisa Mtendaji, wananchi wengine waliokutwa na hatia kama
hiyo ni Rajabu Shomari, Mbwana Kandu, Rajabu Mussa, na Amani Kassim Issa
ambao kwa pamoja walinusurika kwenda jela baada ya kulipa faini ya Sh
200,000 kila mmoja.
Katika Shule ya Sekondari ya Kutwa ya Marumba, wanafunzi walioanza
kidato cha kwanza mwaka 2013 walikuwa 64, lakini waliobaki ambao
wameanza kufanya mitihani ni wanafunzi 17 akiwamo msichana mmoja kati ya
12. Shule ya Sekondari Mchoteka iliyopo Kata ya Mchoteka wilayani humo,
wanafunzi walioteuliwa kuanza masomo ya kidato cha kwanza mwaka 2013
walikuwa 100 hata hivyo, waliobaki ni wanafunzi 21 katika shule hiyo.
Comments
Post a Comment