BAJETI MPYA YA MWAKA HII HAPA
SERIKALI imepanga kutumia Sh trilioni 32.946 katika bajeti yake ya
mwaka 2017/2018, ikiwa imeongezeka kutoka Sh trilioni 29.5 ya mwaka
2016/2017 na kutaja maeneo
ya kipaumbele kuwa ni pamoja na kuzingatia
miradi ya kufufua kiwanda cha General Tyre cha Arusha na kuendeleza
maeneo ya viwanda vidogo.
Sambamba na hilo, serikali imebainisha mikakati yake ya kudhibiti
matumizi, ambapo sasa itahakikisha mikataba inayoingiwa na serikali na
taasisi zake inakuwa katika shilingi za Tanzania, isipokuwa kwa mikataba
inayohusisha biashara za kimataifa.
Kuhusu kuhamishia shughuli za makao makuu ya serikali Dodoma, mipango
ya ujenzi wa majengo na miundombinu yote ya serikali iliyopangwa
kujengwa Dar es Salaam, itahamishiwa Dodoma.
Akiwasilisha bungeni jana mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa
kwa mwaka 2017/2018 na mwongozo wa kuandaa mpango na bajeti ya serikali
kwa mwaka 2017/2018, Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango
alisema kati ya Sh trilioni 32.946, Sh trilioni 19.782 zitatengwa kwa
ajili ya matumizi ya kawaida.
Comments
Post a Comment