CHINA WAMEONYESHA NDEGE ZAO MPYA ZA KIVITA HIZI HAPA
China imeonyesha
hadharani ndege zake mpya za kivita aina ya J-20 ambazo zina uwezo wa
kujificha na kukosa kuonekana kwenye mitambo ya rada.
Ndege mbili za aina hiyo zilipaa angani kwa sekunde 60 wakati wa maonesho ya ndege ya Zhuhai katika mkoa wa Guangdong.
Maonesho hayo huwa makubwa zaidi nchini humo na huwakutanisha waundaji na wanunuzi wa ndege.
Ndege hizo zinatazamwa na wengi kama ishara ya hamu ya Beijing kuboresha na kuimarisha uwezo wake kijeshi.
Rais wa China Xi Jinping anataka kuimarisha majeshi ya nchi yake
huku taifa hilo likiendelea kudhihirisha ubabe sana kuhusu umiliki wa
maeneo ya bahari Kusini na Mashariki mwa China.
Ndege hizo za J-20 zimeundwa na kampuni ya Chengdu
Aircraft Industries Group, ambayo ni kampuni tanzu ya shirika la ndege
la China ambalo kwa Kiingereza hufahamika kama Aviation Industry
Corporation of China.
Baadhi wamelinganisha ndege hizo na ndege aina ya F-22 Raptor za Lockheed Martin.
Comments
Post a Comment