KANISA LA WATU WEUSI LACHOMWA MOTO HUKO MAREKANI
Polisi katika jimbo la Marekani la
Mississippi wanasema wanachunguza uhalifu wa chuki baada ya Kanisa
linalotumiwa na watu weusi kuteketezwa na kisha kuchorwa maneno ya
kusema: "Mpigie kura Trump".
Kanisa hilo linalopatikana eneo la Greenville lilijengwa miaka 111 iliyopita.
Msimamizi wa kituo cha zima Moto alisema kuwa moto katika Kanisa la Hopewell Missionary Baptist Church uliwashwa makusudi.
Shambulio hilo limetokea wiki moja kabla ya uchaguzi wa urais kufanyika Jumanne wiki ijayo.
Maafisa wanasema ujumbe ulioandikwa kwenye jumba hilo ni wa kuzua hofu.
Meya
wa Greenville, Mississippi amesema kisa hitendo hicho ni cha "chuki na
woga" na s"shambulio la moja kwa moja dhidi ya uhuru wa watu kuabudu".
Kisa
hicho kinawakumbusha watu kuhusu visa vya kuchomwa moto kwa makanisa ya
watu weusi miaka ya 1950 na 1960, watu weusi waliokuwa wanapigania haki
zao.
Maafisa wa FBI wakishirikiana na wachunguzi wa jinai wa jimbo la Mississippi kwa sasa wanaendelea na uchunguzi.
Comments
Post a Comment