LEMI ATIWA MBALONI KWA MALA YA PILI
WAKATI Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imetoa hati ya kukamatwa kwa
Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu (Chadema) kwa sababu amekiuka
masharti
ya dhamana, Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema (Chadema),
amekamatwa na Polisi kwa mahojiano ya kutoa lugha za uchochezi.
Lema alikamatwa usiku wa kuamkia jana akiwa mkoani Dodoma, kuhudhuria vikao vya Bunge na kusafirishwa hadi Arusha.
Akizungumza jana na waandishi wa habari ofisini kwake Kamanda wa
Polisi Mkoani Arusha, Charles Mkumbo, alisema Lema yuko mahabusu kwa
mahojiano mpaka watakapomaliza na kumfikisha mahakamani, kujibu makosa
anayokabiliwa nayo.
Mkumbo alisema Lema amekuwa akitoa maneno na lugha za uchochezi na
kuzirudia kila mara, hivyo wameona vyema wamweke ndani kwa mahojiano.
“Juzi tulimkamata akitokea Dodoma na tulifanya naye mahojiano na
kumwachia kwa dhamana, lakini kuna baadhi ya makosa hatukuwahi kumhoji,
sasa ndio tumeamua kumhoji,” alisema.
Pamoja na Polisi kutosema ni lugha gani ya uchochezi imetumiwa na
Mbunge huyo kiasi cha kuka matwa, Novemba Mosi mwaka huu Kamanda Mkumbo
akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake, alitaja maneno ya
uchochezi anayodaiwa kuyasema Lema.
Comments
Post a Comment