MADINI MAPYA YAGUNDULIWA TANZANIA
Madini mapya yamegunduliwa nchini Tanzania, katika eneo lenye madini ya kipekee la Manyara, na kupewa jina Merelaniite.
Jina
hilo limetokana na eneo ambalo madini
hayo yalipatikana, Merelani
(Mererani) katika milima ya Lelatema katika wilaya ya Simanjiro katika
eneo la Manyara.
Eneo hilo linafahamika sana kwa madini ya Tanzanite.
Madini
hayo yaligunduliwa na wataalamu kutoka Chuo Kikuu cha Kiteknolojia cha
Michigan cha Marekani, makavazi ya historia asilia ya London, chuo kikuu
cha Di Firenze cha Italia na makavazi ya historia asilia ya Smithsonian
ya Washington.
Wataalamu sita waliofanya uchunguzi, kwenye makala
iliyochapishwa kwenye jarida la Minerals (Madini) wanasema madini hayo
yana vipande vinavyofanana na sharubu vya rangi ya kijivu vya urefu wa
milimita moja hivi, ingawa kuna baadhi vyenye urefu wa hadi mililita 12.
Kipenyo cha vipande hivyo ni mikrometa kadha.
Madini
hayo yanakaribiana na madini ya zoisite (aina ya tanzanite), prehnite,
stilbite, chabazite, tremolite, diopside, quartz, calcite, graphite,
alabandite na wurtzite.
Comments
Post a Comment