MAN CITY YALIPA KISASI KWA BARCELONA
Manchester City wanahitaji kushinda
mechi moja kufika hatua ya muondoano Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya baada ya
kupata ushindi wa kusisimua dhidi ya miamba wa Uhispania Barcelona.
Mechi hiyo ilichezewa uwanja wa Etihad.
Lionel
Messi alifunga bao lake la 90 ligi hiyo ya mabingwa baada ya kupokea
pasi kutoka kwa Neymar na kuwaweka mbele Barca muda wa mapumziko
ulipokuwa unakaribia.
City,
ambao walikuwa wanatafuta ushindi wao wa kwanza dhidi ya Barcelona
katika mechi sita, walianza kudhihirisha ubabe wao kuanzia wakati huo na
frikiki ya Kevin de Bruyne ilimuumbua kipa Marc-Andre ter Stegen dakika
ya 51.
Mpira wa Andre Gomes uligonga mwamba huku Barcelona
wakisaka bao la kusawazisha lakini City walijihakikishia ushindi wa
kusisimua dhidi ya klabu ya zamani ya meneja wao Pep Guardiola zikiwa
zimesalia dakika 16 pale De Bruyne alipompa pasi Jesus Navas naye akatoa
krosi iliyomfikia mshambuliaji Sergio Aguero, kabla ya kumfikia
Gundogan aliyefunga.
City watafuzu kwa hatua ya 16 bora iwapo watashinda Borussia Monchengladbach ugenini Novemba 23.
Comments
Post a Comment