MBOWE AZUA TAHALUKI BUNGENI


Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe

KIONGOZI wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe jana alisababisha taharuki katika kikao cha Bunge baada ya kuzusha tuhuma za rushwa kwa wabunge wa CCM katika
kipindi cha maswali na majibu na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa.
Ingawa swali lake hilo lenye tuhuma lilizuiwa kujibiwa na Naibu Spika, Dk Tulia Akson kwa kuwa halikuwa swali la kisera, hoja iliibuliwa tena na wabunge wengine wakati wa kuingia kipindi cha majadiliano, kama miongozo.
Mbowe katika swali lake kwa Waziri Mkuu alituhumu wabunge wa CCM, kupewa rushwa ya Sh milioni 10 kila mmoja na serikali ya chama hicho ili kuupitisha Muswada wa Huduma za Habari unaowasilishwa bungeni leo.
Aidha alidai rushwa hiyo, pia imetolewa kupitisha Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa mwaka 2017/18. Pamoja na tuhuma hizo kutojibiwa na Waziri Mkuu kutokana na muundo wa maswali ya papo kwa hapo kugusa sera, Mbunge wa Momba, David Silinde (Chadema) aliomba mwongozo wa Spika huku akitaka kuundwe Tume Huru ya Kimahakama ya Bunge, kuchunguza tuhuma hizo.
Naye Mbunge wa Chemba, Juma Nkamia (CCM) alisimama na kuomba mwongozo, na kumtaka Mbowe athibitishe tuhuma hizo au achukuliwe hatua.

Comments