MKE WA LEMA KORTINI KWA KUTOA LUGHA YA MATUSI
MKE wa Mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini, Godbless Lema, Neema Lema
(33) amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha na kuunganishwa
katika
kesi ya mume wake ya kumtukana Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho
Gambo kuwa ni shoga.
Akimsomea mashitaka hayo kwa mara ya kwanza, Wakili wa Serikali,
Blandina Msawa mbele ya Hakimu Augustino Rwezile, alidai kuwa kati ya
Agosti 20, mwaka huu ndani ya Arusha, Neema ambaye ni mkazi wa Njiro
alimtumia ujumbe wa simu ya kiganjani mkuu huyo wa mkoa wenye lugha ya
matusi, huku akijua ni kosa kisheria.
Alidai mtuhumiwa huyo alituma ujumbe kutoka namba 0764 xxx 747 na
0756 551 918 kwenda namba 0766 XXX 575 uliokuwa ukidai, “Karibu,
tutakudhibiti kama Uarabuni wanavyodhibiti mashoga.”
Mshitakiwa alikana shitaka hilo na yupo nje kwa dhamana hadi Novemba 15, mwaka huu itakapotajwa tena kesi hiyo.
Comments
Post a Comment