MUHIMBILI YAPATA SHILINGI BILIONI 4.6 YASEMA HAPA KAZI TUH
HOSPITALI ya Taifa Muhimbili (MNH) imekuwa ikikusanya mapato ya Sh
bilioni 4.6 kwa mwezi kuanzia Desemba mwaka jana hadi kufikia Oktoba
mwaka huu, ikiwa ni ongezeko la asilimia 100.
Fedha ni zaidi ya wastani wa Sh
bilioni 2.3 ilizokuwa ikizalishwa na
hospitali hiyo kwa kipindi kama hicho kuanzia Dasemba 2014 hadi Oktoba
2015.
Sambamba na ongezeko hilo, pia huduma za vipimo vya MRI, CT –Scan,
X-Ray na Ultra Sound zimeongezeka ambapo katika kipindi cha mwaka mmoja
sasa, jumla ya wagonjwa waliopimwa kwa kutumia vipimo hivyo wamefikia
55,073 ukilinganisha na kipindi kama mwaka uliopita ambapo wagonjwa
waliopimwa walikuwa 23,989.
Akitoa taarifa ya mafanikio ya mwaka mmoja madarakani ya Serikali ya
Awamu ya Tano jana jijini Dar es Salaam, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano
ya Umma cha hospitali hiyo, Aminiel Eligaesha alisema hivi sasa
mwelekeo wa mapato ya MNH kuanzia Julai 2016 hadi Oktoba 2016 unaonesha
hospitali hiyo imezalisha Sh bilioni 4.6 kwa mwezi na kusema hayo ni
mafanikio makubwa kuwahi kupatikana katika kipindi kifupi cha miezi
miwili.
Comments
Post a Comment