RAIS MAGUFULI AZINDUA BARA BARA HUKO KENYA

 Rais John  Magufuli akiwa na mwenyeji wake Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta, Naibu Rais wa Kenya, William Rutto pamoja na viongozi wengine, wakikata utepe kuashiria ufunguzi wa barabara ya kupunguza msongamano ya Nairobi Southern Bypass jijii Nairobi nchini Kenya jana. (Picha na Ikulu)
RAIS John Magufuli na Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya wamezindua barabara ya Southern By-pass iliyojengwa kwa lengo la kupunguza msongamano
wa magari katika Jiji la Nairobi, nchini Kenya.

Kwa mujibu wa taarifa ya Ikulu ya Tanzania, sherehe ya uzinduzi wa barabara hiyo yenye urefu wa kilometa 28 na inayounganisha maeneo mbalimbali ya Jiji la Nairobi, imefanyika katika eneo la Kareni nje kidogo ya Jiji la Nairobi jana.
Akizungumza katika sherehe hiyo, Rais Magufuli amempongeza Rais Kenyatta na serikali yake kwa kujenga barabara hiyo ambayo sio tu itawasaidia wananchi wa Kenya, bali pia itawasaidia wananchi wa Afrika Mashariki wanaotumia barabara zinazopitia Nairobi.

Comments