SELFII YA MPONZA BINTI HUYU AKIGONGA NA POLISI
wanafunzi mmoja wa chuo kikuu nchini
Marekani aligongesha gari lake kwa lile la polisi, wakati akijipiga
picha za selfie huku akiendesha gari.
Miranda Rader mwenye umri wa
miaka 19, aligonga gari polisi alipokuwa akimtumia mpenzi wake picha
za utupu kupitia kwa mtandao wa Snapchat.
Ajali hiyo iliyotokea eneo la Bryan umbali wa kilomita 160 Kaskazini mwa mji wa Houston, ilisababisha mfuko wa hewa kuchomoka
Mwanafunzi huyo pia alipatikana na chupa ya mvinyo ndani ya gari lake kwa mujibu wa polisi. Hakuna mtu aliyejeruhiwa.
Polisi
ambaye gari lake liligongwa alikaribia gari la Bi Rader na kumpata
akijaribu kuvaa nguo. Alipoulizwa mbona, alijibu akisema kuwa alikuwa
akijipiga picha za selfie za kumtumia mpenzi wake.
Alikamatwa kwa kushukiwa kuendesha gari akiwa mlevi na kuachiliwa kwa dhamana ya dola 2000.
Comments
Post a Comment