TFF YAPOKEA BILION 1 KUTOKA KWA FIFA
SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) kuanzia mwakani litapata ruzuku ya
kiasi cha dola 500,000 sawa na Sh bilioni 1 kwa ajili ya maendeleo ya
soka la wanawake na vijana.
Akizungumza na waandishi wa habari jana, Ofisa Habari wa TFF, Alfred
Lucas alisema awali walikuwa wakipata dola 250,000 kutoka Shirikisho la
Kimataifa la Soka (Fifa), lakini kuanzia mwakani dau limepanda mara
mbili.
“TFF kuanzia Julai mwakani tutakuwa tukipata ruzuku ya dola 500,000
ikiwa mara mbili ya zile za awali kwa ajili ya kuendeleza soka la vijana
na wanawake na hii imetokana na maendeleo mazuri ya soka hilo hapa
nchini,“ alisema Lucas.
Pia Lucas alisema kutokana na timu za vijana na wanawake kupata
ruzuku hiyo ndio maana timu hizo zinasafiri kucheza mashindano
mbalimbali.
“Mtakumbuka Kilimanjaro Queens walikwenda kwenye mashindano ya
Chalenji ghafla kwa sababu ya ruzuku hiyo na tunashukuru walifanya
vizuri, jambo ambalo limesaidia Tanzania kujulikana kwenye medani ya
kimataifa kwa ajili ya soka la wanawake na vijana”, alisema Lucas.
Lucas alisema Twiga Stars imerudi jana usiku kutoka Cameroon, ambapo
ilicheza michezo miwili ya kirafiki huku ikishinda mmoja na kupoteza
mwingine.
Hatahivyo, wadau wa soka wamekuwa na wasiwasi kama kweli fedha hizo
zilikuwa zikitumika vizuri, kwani timu za wanawake mara kadhaa zilikuwa
zikilalamikia posho na mambo mengine
Comments
Post a Comment