WAFANYA KAZI HEWA SASA HII SIFA
WATUMISHI hewa 19,629 wamebainika kuwapo nchini tangu uhakiki
ufanyike; na kama wangelipwa, serikali ingepoteza Sh bilioni 19.7 kwa
mwezi.
Aidha, kutokana na hali hiyo, serikali imechukua hatua za kinidhamu
dhidi ya watumishi 1,663 kutoka katika taasisi zake kwa watumishi
waliohusika na kuwepo kwa watumishi hewa na kati ya hizo, watumishi 638
wamefunguliwa mashtaka polisi.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na
Utawala Bora, Angella Kairuki, alisema bungeni mjini hapa jana kuwa
serikali ingepata hasara hiyo, endapo watumishi hao hewa wangelipwa kwa
mwezi.
Akitoa mfano wa halmashauri mbili, Kairuki alisema Kinondoni imekutwa
na watumishi hewa 107 na kama wangelipwa ingepoteza Sh bilioni 1.279 na
kwa Halmashauri ya Kishapu waligundulika 73 na wangelipwa Sh milioni
543.
Comments
Post a Comment