WANAOJICHUBUA WANA MATATIZO YA KISAIKOLOJIA
WATU wanaopenda kujibadilisha miili na ngozi zao kwa kutumia vipodozi
vyenye kemikali za kujichubua na kubadilisha mwonekano wa sehemu za
maumbile yao wametajwa kuwa miongoni mwa watu wanaosumbuliwa na matatizo
ya kisaikolojia.
Mwenyekiti wa Kigoda cha Mwalimu Nyerere, Profesa Penina Mlama alisema wanawake na wanaume ambao wanatumia vipodozi hivyo wana matatizo ya kujiamini, hivyo huchukua uamuzi wa kujibadilisha.
Aliyasema hayo jana wakati akizungumza kwenye mkutano wa kimataifa kati ya Shirika la Codersia na Majumuhi (Pan African) ya Kigoda cha Mwalimu Nyerere wa kujadili mabadiliko ya mwili ambayo yamekuwa yakifanywa na watu mbalimbali.
Alisema watu wamekuwa wakifanya mabadiliko kwa kujichubua, kujichora mwilini (tattoos), kuongeza maumbile bila kujua kuwa kuna madhara makubwa ya kufanya hivyo.
Comments
Post a Comment