WAPAKISTANI WATATU WAHUKUMIWA MIAKA MINNE JELA
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imewahukumu raia watatu wa Pakistan,
kifungo cha miaka minne jela au kulipa faini ya Sh milioni 125 baada ya
kupatikana na hatia ya kuingilia mtandao wa mawasiliano na kuisababishia
serikali hasara ya Sh milioni 145.
Hakimu Mkazi Mkuu, Respicius Mwijage, alitoa hukumu hiyo baada ya
washtakiwa, Hafees Irfan, Mirza Irfan Baig na Mirza Rizwani Baig, kukiri
makosa yao.
Akitoa adhabu hiyo, Hakimu Mwijage alisema, washtakiwa wamepatikana
na hatia ya makosa manne na katika kila kosa watalipa faini ya Sh
milioni tano au kutumikia kifungo cha mwaka mmoja jela, ambayo ni sawa
na faini ya Sh milioni 20 au kifungo cha miaka minne jela.
Aidha, alisema kwa sababu mashtaka yanahusisha kuisababishia hasara
Mamlaka ya Mawasiliano (TCRA), kila mshtakiwa anatakiwa kulipa faini ya
Sh milioni 35, pia washtakiwa wakimaliza kutumikia vifungo vyao, warud
ishwe nchini kwao na vifaa walivyokutwa navyo vitakuwa mali ya serikali.
Alidai, washtakiwa walitoka Pakistan na kwenda maeneo mbalimbali
ikiwemo Arab Emirates, Malaysia, Msumbiji kwa ajili ya kutumia vifaa
hivyo, pia waliingia nchini katika tarehe tofauti na kufikia kwenye
chumba namba 905 katika Hoteli ya Butterfly iliyopo Kariakoo, Dar es
Salaam.
Comments
Post a Comment