WATANO WANASWA KESI YA KIFO CHA MASHALI

Image result for thomas mashali
WATUHUMIWA watano wa mauaji ya bondia Thomas Fabian Mashali maarufu ‘Simba Asiyefungika’ wamekamatwa leo Kimara mjini Dar es Salaama.
Kaka wa marehemu, Emmenuel Mashali ameiambia
CHANZO BINZUBERY >>>>KAKWAYA100 leo kwamba wamefanikiwa kuwasaidia Polisi kuwatia nguvuni watuhumiwa watano wa mauaji wa ndugu yao.
“Tupo na Polisi huku Kimara tunawasaidia kuwapata watuhumiwa. Tumefanikiwa kuwakamata watuhumiwa watano, na tumewaleta kituo kidogo cha Polisi Kimara. Lakini watapelekwa kituo kikubwa cha huku (Mbezi). Baada ya hapo ndio watapelewa mahakamani. Wawili tumewakamata KImara Bonyokwa na watatu KImara Salanga,”amesema Emmanuel Mashali.


Hata hivyo, alipoulizwa Kamanda wa Polisi wa Kanda maalum ya Kinondoni, Dar es Salaam, Susan Kaganda amesema hawawezi kusema chochote kwa sasa hadi hapo watakapokamilisha uchunguzi wao.

Hadi anakutwa na umauti, Mashali alikuwa amepigana jumla ya mapambano 26 ya ngumi za kulipwa akishinda 19, kushindwa matano, sare moja na moja lilifutwa ulingoni.
Enzi za uhai wake, Mashali alikuwa mkali kweli ulingoni akishinda mataji tofauti kuanzia la Afrika Mashariki na KatiOktoba 14, mwaka 2012 kwa kumpiga Med Sebyala wa Uganda kwa pointi ukumbi wa Friends Corner, Dar es Salaam.
Akalitetea taji hilo kwa kumpiga Mkenya Bernard Mackoliech Januari 12, mwaka 2013, ukumbi wa Friends Corner, hivyo kupata nafasi ya kwenda kuwania taji la IBF Afrika, ambalo hata hivyo alilikosa kwa kupigwa na Mtanzania mwenzake, Francis Cheka Mei 1, mwaka 2013 kwa Knockout (KO) raundi ya saba ukumbi wa PTA, Dar es Salaam.

Comments