WATUHUMIWA WA MAUWAJI YA WATAFITI WALIOCHOMWA MOTO WAPANDISHA KIZIMBANI


 

WASHiTAKIWA 13 wa mauaji ya watafiti watatu wa Kituo cha Utafiti wa Kilimo cha Selian (SARI) jijini Arusha, wamesomewa upya mashitaka mapya jana.

Kila mshitakiwa anakabiliwa na mashitaka matatu ya mauaji. Awali, walisomewa shitaka moja la kuwaua watu watatu kwa wakati mmoja.
Washitakiwa hao ni Mwenyekiti wa Kijiji cha Iringa Mvumi, Albert Chimanga (58), Cecilia Chimanga (34), Sostheness Mseche (35) ambaye ni Mwinjilisti, Julius Chimanga (35), David Chimanga (44), Dorca Mbehu (55), Edna Nuno (47), Grace Msaulwa (41), Juma Madehe (44), Lazaro Kwanga (35), Yoram Samamba (55), Edward Lungwa (39) na Simon Samamba (22).
Mbele ya Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Dodoma Mjini, Joseph Fovo, washitakiwa walisomewa mashitaka na Mwendesha Mashtaka wa Serikali, Beatrice Nsana ambaye katika shitaka la kwanza, ilidaiwa Oktoba mosi mwaka huu, katika kijiji cha Iringa Mvumi wilaya ya Chamwino mkoani Dodoma, washtakiwa kwa pamoja walimuua Nicas Magazine

Comments