21 KORTINI KWA KUFANYA VURUGU CHUNYA
Askari wakiwa Doria |
Jumla
ya watuhumiwa 21 akiwemo mwanamke mmoja wamefikishwa katika mahakama ya
Wilaya ya Chunya kwa kuhusika na vurugu zilizotokana na wananchi
wilayani humo kuvamia kituo cha polisi kwa lengo la kuwatoa watuhumiwa
wa mauaji ili kuwaadhibu.
Watu hao waliofikishwa mahakamani ni sehemu ya watuhumiwa 41 waliokamatwa, kati yao wanaume wakiwa 34 na wanaweke 7 baada ya vurugu zilizotokea jana na kusabababisha jumla ya watu 7 kujeruhiwa wakiwemo askari polisi wanne, na wananchi watatu huku mwananchi mmoja aliyefahamika kwa jina la AMOKE MBILINYI (25) akifariki dunia.
Taarifa
ya Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya imeeleza kuwa tukio hilo limetokea
mnamo tarehe 18.12.2016 majira ya saa 11:45 asubuhi katika Kituo cha
Polisi Makongolosi kilichopo Kata ya Makongolisi, Wilayani Chunya ambapo
kundi la wananchi walioamua kujichukulia sheria mkononi walivamia kituo
hicho cha Polisi na kufanya fujo kwa kuwarushia mawe hovyo askari.
Kwa
mujibu wa jeshi hilo, lengo la uvamizi huo ilikuwa ni kuwatoa
watuhumiwa wawili waliofahamika kwa majina ya 1. ERASTO ROBERT, mkazi wa
Kilombero na 2. BASI LINUS mkazi wa Makongolosi waliokuwa wanakabiliwa
na kosa la mauaji kwa lengo la kuwatoa nje na kuwauawa kwa kuwachoma
moto.
Aidha
wananchi hao walifunga barabara ya Chunya/Makongolosi kwa kuweka mawe
makubwa na magogo hali iliyosababisha usumbufu mkubwa wa watumiaji
wengine wa barabara hiyo.
Jeshi hilo limesema thamani ya uharibifu bado kufahamika na hali imerejea kuwa shwari
Awali
mnamo tarehe 11.12.2016 majira ya saa 23:20 katika Kitongoji cha
Manyanya, mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la JACOB BROWN Mkazi wa
Manyanya alivamiwa na watu wasiojulikana akiwa peke yake shambani kwake
na kuuawa ambapo Polisi walifanya msako na kuwakamata watu hao wawili
kwa mahojiano zaidi kuhusiana na tukio hilo.
Mbeya RPC Dhahiri Kidavashari |
Comments
Post a Comment