3 WANUSURIKA KUUAWA HANANG
Watu watatu kutoka Jijini Arusha wamenusurika kuuwawa na wananchi wenye
hasira kali katika kijiji cha Mogitu wilayani Hanang, baada ya kukutwa
wakiharibu miundo mbinu ya Tanesco na kusababisha hasara ya zaidi ya
milioni kumi kwa Shirika hilo la umeme.
Transfoma |
Wananchi wa kijiji hMogitu wameeleza hali halisi ya
tukio la kuwakamata wahusika wa kuharibu miundo mbinu ya Tanesco na
hivyo kupelekea kilio hata kwananchi kukosa nishati ya umeme ambayo
wamesema kuwa wanategemea katika kuendesha mitambo yao ya kuvuta maji
kwaajili ya matumizi ya kila siku pamoja na kunywesha mifugo yao.
Marietha Chimwenda ni meneja wa shirika la umeme tanesco wilayani
hanang ambapo kuwa atahakikisha wananchi wanarejeshewa huduma mara moja.
Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa manyara kamishina msaidizi Franci Masawe amethibitisha kukamatwa kwa wahusika wa tukio hilo.
Kwa mujibu wa kamanda masawe majina ya watuhumiwa yanahifadhiwa kwa sababu za kiuchunguzi.
Comments
Post a Comment