41 WAFARIKI KWA KUNYWA SABUNI YA KUOGEA
Takriban watu 41 wamefariki katika mji wa Serbia wa Irkutsk baada ya kunywa sabuni ya kuogea, kulingana na mamlaka ya Urusi.
Sabuni
hiyo ilio majimaji ilitumika kama pombe kulingana na kamati ya
uchaguzi nchini Urusi. Watu wengine 16 wako katika hali mbaya.
Tayari watu wawili wanazuiliwa kufuatia kisa hicho huku polisi wakionda chupa za sabuni hyo katika maduka.
Wachunguzi wanasema onyo kwamba sabuni hiyo haikufaa kutumika kama kinywaji lilidharauliwa.
Bidhaa hiyo ilikuwa na methanol, kemikali inayotumika kuyeyusha barafu.
Hali ya tahadhari imetangazwa katika eneo hilo la Irkutsk, na wachunguzi wa Urusi wameanzisha uchunguzi.
Vyombo
vya habari vya Urusi vimeripoti kwamba waathiriwa walikuwa watu
masikini ,walio na umri kati ya 35 na 50 na kwamba hawakuwa wakinywa kwa
pamoja.
Bidhaa za nyumbani mara nyengine huonekana kuwa rahisi
kwa matumizi mbadala ya pombe katika eneo hilo lililokuwa muungano wa
Usovieti.
Huku visa vya sumu ya pombe vikiwa vya kawaida, kisa hiki ndicho kibaya zaidi kuwahi kutokea kwa miaka kadhaa.
Comments
Post a Comment