AJIBU AANZA KUFUNGA HUKO MISRI
MSHAMBULIAJI chipukizi wa kimataifa wa Tanzania, Ibrahim Hajib Migomba leo amefunga bao moja timu ya Haras El Hodoud ikishinda 4-0 katika mchezo wa kirafiki mjini Alexandria, Misri.
Akizungumza na Bin Zubeiry Sports – Online leo, Hajib amesema kwamba amefunga bao moja timu yake ikishinda 4-0 Uwanja wa Haras Hodoud mjini Alexandria.
Hata hivyo, Hajib hajui wamecheza na timu gani wala wafungaji wa mabao mengine ya timu hiyo.
“Ninamshukuru Mungu leo tumecheza mechi ya kirafiki tumeshinda 4-0 na mimi nimefunga bao moja,”amesema.
Tayari imeripotiwa Hajib amefuzu majaribio ikiwa pamoja na vipimo vya afya katika klabu ya Haras El Hodoud ya Ligi Kuu ya Misri.
Sasa kinachosubiriwa ni makubaliano tu baina ya Hodoud na Simba SC ili Hajib ahamie rasmi Misri.
Hajib aliondoka nchini Alhamisi ya wiki iliyopita kwenda Misri kwa majaribio ya kucheza soka ya kulipwa baada ya kupewa baraka zote na uongozi wa Simba.
Mshambuliaji huyo ameonyesha kiu ya kweli ya kutaka kucheza nje ya Tanzania, kwani katikati ya mwaka huu alikwenda Afrika Kusini kwa majaribio pia, ambako pamoja na kuripotiwa kufuzu katika klabu ya Lamontville Golden Arrows FC ya Ligi Kuu ya ABSA nchini humo.
Comments
Post a Comment