BARROW ATAKA JAMMEH AACHIE NCHI

Rais wa Gambia Yahya Jammeh
Muungano unaongozwa na rais mteule wa Gambia Adama Barrow, umemtaka kiongozi wa miaka mingi wa nchi hiyo Yahya Jammeh, aondoke madarakani na kukabidhi mamlaka.

"Nafikiri anastahili kuondoka madarakani ameshindwa kwenye uchaguzi, hatutaki kupoteza wakati, tunataka nchi hii iendelee mbele." Barrow alinukuliwa na shirika la AFP.
Bwana Jammeh amesema kuwa ana mipango ya kupinga matokeo hayo katika mahakama ya juu, baada ya kubadilisha mawazo siku ya Ijumaa baada ya kutangaza kukubali kushindwa awali.

Comments