BOSI JAMII FORUM ARUDISHWA KEKO HADI JUMATATU
Maxence Melo |
Makosa hayo ni kuendesha na kumiliki tovuti ambayo haijasajiliwa hapa nchini na kuzuia uchunguzi wa polisi kwa mujibu wa Sheria ya Makosa Kimtandao.
Melo anadaiwa kusimamia anwani ya mtandao ambayo haijasajiliwa nchini Tanzania kinyume na kifungu 79(c) cha Sheria za Mawasiliano ya Elektroniki na Posta ya mwaka 2010, pamoja na kanuni za anwani za mtandaoni nambari 428 za mwaka 2011.
Nyaraka za mashtaka zinasema anwani ya mtandao ya jamiiforums.com ambayo haijasajiliwa chini ya kikoa cha anwani za Tanzania cha .tz.
Kwenye kosa jingine, ameshtakiwa kuzuia uchunguzi kinyume na kifungu 22(2) cha Sheria za Uhalifu wa Kimitandao ya mwaka 2015.
Nyaraka za mahakama zinasema "akiwa anafahamu kwamba jeshi la polisi lilikuwa linafanya uchunguzi wa jinai kuhusu mawasiliano ya kielektroniki kwenye mtandao wake, na akiwa na nia ya kuzuia uchunguzi, alikataa kutii agizo la kufichua maelezo aliyo nato."
Amepelekwa gereza la Keko mpaka Jumatatu.
Comments
Post a Comment