BOSI NIMR UTEUZI WAKE WATENGULIWA MRITHI ATATANGAZWA
Dkt. Mwele Malecela |
Taarifa
kutoka IKULU inasema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John
Pombe Magufuli, tarehe 16 Desemba, 2016 ametengua uteuzi wa Mkurugenzi
Mkuu wa Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR) Dkt.
Mwele Malecela.
Uteuzi wa Mkurugenzi Mkuu wa NIMR atakayejaza nafasi iliyoachwa wazi na Dkt. Mwele Malecela utatangazwa baadaye.
December
15 2016 Dr. Mwele alinukuliwa na vyombo vya habari akizungumza kuhusu
uwepo wa ugonjwa wa ZIKA Tanzania na kwamba asilimia 15 ya waliopimwa
walikutwa na virusi vya ugonjwa huo ambapo hata hivyo taarifa hizo
zilikanushwa na wizara ya afya jana.
Comments
Post a Comment