BUNGE LA CUBA LAPITISHA OMBI LA FIDEL CASTRO
Bunge la Cuba limepitisha kwa kauli
moja katazo la kuzuia majengo, mitaa au minara ya kumbukumbu kupewa jina
la mwanamapinduzi mkongwe nchini humo Fidel Castro, ambaye alifariki
dunia mwezi uliopita.
Rais wa Cuba Raul Castro amesema kaka yake
alipinga mitindo hiyo na hadi kufikia hatua ya kuliwasilisha suala hilo
bungeni kupigiwa kura.Fidel Castro aliongoza mapinduzi ya Cuba, ambayo mwaka 1959, waliuondoa madarakani utawala uliokuwa ukiungwa mkono na Marekani.
Aliifanya nchi hiyo kuwa ya Kikomunisti na kubaki kwenye utawala kwa takriban miongo mitano.
Comments
Post a Comment