FRANCIS CHEKA APIGWA (KO) HUKO INDIA

 Image result for FRANCIS CHEKA

BONDIA Francis Cheka wa Tanzania amepigwa kwa Knockout (KO) raundi ya tatu na Vijender Singh Uwanja wa Thyagaraj mjini New Delhi, India usiku wa Jumamosi.

Kwa ushindi, huo Singh amefanikiwa kutetea taji lake la ubingwa wa WBO Asia Pacific uzito wa Super Middle.
Baada ya kummaliza bingwa huyo wa zamani wa dunia, Singh alisema; "Nilifanya mazoezi makali mjini Manchester kwa miezi miwili kwa ajili hii. Nawashukuru makocha wangu wote kwa jitihada zao kwangu,".
Aidha, Singh alisema Cheka aliongea sana kabla ya pambano, lakini yeye aliamini juu ya uzito wa ngumi zake na amefanikiwa kuzitumia vizuri kumshikisha adabu Mtanzania.

 Image result for FRANCIS CHEKA

Vijender Singh akizipiga na Cheka Uwanja wa Thyagaraj mjini New Delhi, India usiku wa Jumamosi 

Baada ya kupigwa, Cheka atapanda tena ulingoni Desemba 25 mwaka huu kuzipiga na Abdallah Pazi ‘Dulla Mbabe’ katika pambano la raundi 10 liisilo la ubingwa Uwanja wa Ndani wa Taifa, Dar es Salaam.
Kabla ya kupigwa na Singh, mara ya mwisho Cheka alipanda ulingoni Februari 27 mwaka huu alimpomshinda kwa ponti Geard Ajetovic wa Serbia viwanja vya Leaders Club, Kinodoni, Dar es Salaam na kutwaa taji la WBF Intercontinental uzito huo wa Super Middle.
Na alishinda pambano hilo akitoka kupigwa na Thomas Mashali (sasa marehemu) Desemba 25 Uwanja wa Jamhuri, Morogoro.

Comments