CHEKA AZUNGUMZIA SABABU YA KUPIGWA INDIA
Bondia Mtanzania Francis Cheka ambaye mwishoni mwa wiki alipoteza
pambano lake nchini India alilopigana na raia wa nchi hiyo Vijender
Singh, ameibuka na kusema kuwa mpinzani wake huyo hakumpiga, ila
alibebwa na mwamuzi.
Cheka amesema katika raundi hiyo ya tatu, alipata tatizo katika kifaa chake cha kulinda meno kwa kuwa alikuwa akisumbuliwa na kikohozi, na wakati anakifanyia marekebisho, ndipo mwamuzi akatangaza mshindi, bila kumuuliza Cheka mwenyewe kama alikuwa anaendelea au la.
“Tatizo nilikuwa nakohoa, nilijiandaa vizuri kumpiga yule Vijender,” alisema Cheka.
Pia katika mtandao wake wa Instagram aliandika:
Pale ambapo matokeo yamepangwa, tunaenda kukamilisha ratiba tu, Refa unaona mouth guard imetoka na unaendelea kuchezesha… Watanzania nadhani mmeona, tusiwage wanyonge kwao na kwetu pia… Nadhani nimeliwakilisha taifa vyema, kuitangaza Morogoro, Tanzania, Kiswahili na Kimakonde pia.

Comments
Post a Comment