CHRISTINE LAGARDE WA IMF AKUTWA NA MAKOSA
Mkuu wa shirika la fedha duniani IMF
Christine Lagarde, amepatikana na makosa ya kutomakinika wakati
alipotoa malipo makubwa ya fidia miaka 8 iliyopita, wakati akiwa waziri
wa fedha wa Ufaransa.
Kesi hiyo ilisikilizwa na mahakama maalum iliyoamua kwamba haitomwadhibu wala kumpa rekodi ya uhalifu.Lagarde alilipa pesa hizo katika mpango wa upatanishi, ambapo bwanyenye kwa jina Bernard Tapie, alipokea zaidi ya dola milioni 400.
Bodi ya IMF itafanya kikao kutathmini matokeo ya kesi hiyo, huku mawakili wa Lagarde wakisema kwamba watakata rufaa.
Comments
Post a Comment