DANGOTE ATINGA IKULU APIGA STORY NA MAGUFULI
Mmiliki wa kiwanda cha cha Saruji cha Dangote Alhaji
Aliko Dangote
|
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli
amekutana na kufanya mazungumzo na Mmiliki wa Kiwanda cha Saruji cha Dangote
kilichopo Mtwara, Alhaji Aliko Dangote.
Katika mazungumzo hayo, Rais Magufuli amemhakikishia
mfanyabiashara huyo kuwa serikali ya Tanzania itaendelea kuweka mazingira
mazuri kwa wawekezaji wote nchini katika kutimiza lengo lake la kuwa na
Tanzania ya Viwanda.
Rais Magufuli amesema kuhusu kiwanda cha kuzalisha Saruji cha
Dangote kilichopo Mkoani Mtwara hapakuwa na tatizo lolote ila kulikuwa na watu
ambao walitaka kujinufaisha binafsi kupitia mradi huo kwa kufanya
biashara za ujanja kitu ambacho serikali yake haikiruhusu.
Kwa upande wake mmiliki wa Kiwanda cha kuzalisha Saruji cha
Dangote, Alhaji Aliko Dangote ameshangazwa na baadhi ya vyombo vya habari kudai
kuwa amefunga kiwanda kwa sababu amekatazwa kuagiza makaa ya mawe toka nje ya
Tanzania kitu ambacho amesema hakiingii akilini kwa sababu makaa ya mawe ya
Tanzania ni rahisi na yana ubora kuliko kuagiza nje
|
Comments
Post a Comment