DR CONGO YASITISHA LIGI KUU
Ligi ya kandanda nchini Jamhuri ya
Kidemokrasia ya Congo (DR Congo) imesitishwa kwa muda usiojulikana
kutokana na sababu za kiusalama.
Serikali ililitaka shirikisho la soka nchini humo kusitisha mechi za ligi kuanzia Alhamisi.
Hatua
hiyo imetokea huku wasiwasi ukiendelea kwamba huenda kukatokea vurugu
muhula wa Rais Joseph Kabila utakapofikia kikomo wiki ijayo.
"Hali iliyopo nchini huenda ikafika viwanjani," Barthelemy Okito, katibu mkuu wa wizara ya michezo alisema.
Majuzi wakati wa mechi, mashabiki walisikika wakiimba kwamba muhula wa Kabila unamalizika.
Kabila
alitakiwa kung'atuka 19 Desemba lakini amesema anapanga kusalia
madarakani hadi Aprili 2018, wakati ambao serikali inasema itaweza
kufanya uchaguzi ambao ulikuwa umepangiwa kufanyika mwezi jana.
Comments
Post a Comment