DRC BADO KWAFUKUTA KUHUSU MUAFAKA WA UCHAGUZI MKUU
Joseph Kabila |
Mzozo wa kisiasa unaendelea kutokota
nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo huku muhula wa Rais Joseph
Kabila ukifikia kikomo kwa mujibu wa katiba.
Mazungumzo ya kutafuta suluhu kati ya serikali na upinzani yaliahirishwa wiki iliyopita baada ya kukosekana kwa mwafaka.Mazungumzo hayo yanayoongozwa na maaskofu wa kanisa Katoliki yanatarajiwa kurejelewa Desemba 21.
Kuna wasiwasi kwamba huenda kukatokea maandamano Jumatatu wafuasi wa upinzani wakipinga kuendelea kusalia madarakani kwa Bw Kabila.
Upinzani unamlaumu Rais Kabila ukisema ndiye aliyechangia mzozo wa sasa kwa kujaribu kukwamilia madaraka.
Watu zaidi ya 50 waliuawa kwenye maandamano ya upinzani mwezi Septemba.
Maafisa 3 wa polisi pia waliuawa kwenye maandamano hayo.
Rais Kabila amesema ataendelea kusalia madarakani kwani uchaguzi mkuu haukufanyika ilivyotarajiwa mwezi Novemba na hivyo basi hakuna mrithi aliyechaguliwa.
Wanajeshi na maafisa wa polisi wameweka vizuizi kwenye mji mkuu Kinshasa, kukiwa na wasiwasi wa kutokea tena kwa maandamano na ghasia.
Comments
Post a Comment