EU KUDHIBITI WAHAMIAJI HARAMU NIGER
Umoja wa Ulaya umetoa dola zaidi ya
milioni sita kwa Niger kwa ajili ya kukabiliana na wahamiaji wanaotumia
mipaka ya nchi hiyo kuelekea Ulaya.
Ukanda wa jangwa wa Agadez
nchini Niger hutumika kama njia kuu ya wahamiaji kuelekea nchini Libya
na kisha kutumia bahari ya Mediterranea kuingia Ulaya.
Mpango kama
huo umekwisha fanyika kwa nchi kama Senegal, Ethiopia, Nigeria na Mali
na umoja wa Ulaya unapanga kutafuta nchi nyingine zaidi za Afrika kuweza
kusaidia suala hilo.
Comments
Post a Comment