JOHN DRAMAN MAHAMA AANGUSHWA KWENYE KITI CHA URAIS

Mwanasiasa mkongwe ameshinda uchaguzi wa urais nchini Ghana, ushindi ambao umepokelewa kwa shangwe na nderemo na wafuasi wake.
Nana Akufo-Addo, ameshangilia ushindi wake na kusema taifa hilo sasa ni mwenge wa Demokrasia Afrika Magharibi.
Ameahidi kukabiliana na uchumi uliozorota, suala ambalo lilitiliwa mkazo wakati wote wa kampeni,
Bw Akufo-Addo amesema kuwa ushindi wake ni hatua anayofurahia sana katika maisha yake yote na akaahidi kuwa atafanya kila juhudi kuhakikisha kuwa anatekeleza matakwa ya wananchi wa Ghana.


Rais Mteule Wa Ghana Nana Akufo-Addo


Pia amepongezwa na mshindani wake mkuu, rais John Mahama, aliyeahidi kuheshimu matokeo ya uchaguzi.

Comments