KUMBE MKATA UMEME WA YANGA HAKUCHEZA KWASABABU HII>>>
KIUNGO
mpya wa Yanga, Justin Zulu ameondolewa ghafla katika kikosi cha Yanga
kinachocheza na JKT Ruvu jioni ya leo Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam
kutokana na kutopata kibali cha kufanya kazi nchini.
Mapema jana Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) lilionya mchezaji ambaye hatakuwa na kibaki cha kufanya kazi nchini kutoka Idara ya Uhamiaji hatacheza na Yanga inakuwa ya kwanza kukumbana na kibano hicho.
Yanga inamenyana na JKT Ruvu kuanzia Saa 10:00 jioni ya leo katika mchezo wa kwanza wa mzunguko wa pili Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara na Zulu hayumo kabisa.
Awali, jina lake liliwekwa kwenye kikosi cha watakaoanzia benchi, lakini baadaye likaondolewa na kuwekwa jina la Said Juma ‘Makapu’.
Justin Zulu hachezi leo kutokana na kutopata kibali cha kufanya kazi nchini
Kikosi cha Yanga kinachoanza dhidi ya JKT Ruvu sasa ni; Deogratius Munishi ‘Dida’, Juma Abdul, Mwinyi Haji, Kelvin Yondani, Vincent Bossou, Thabani Kamusoko, Simoni Msuva, Haruna Niyonzima, Donald Ngoma, Amissi Tambwe na Deus Kaseke.
Katike benchi baada ya kuondolewa Zulu wanabaki Ally Mustafa ‘Barthez’, Hassan Kessy, Vincent Andrew, Obrey Chirwa, Juma Mahadhi, Said Juma ‘Makapu’ na Geofrey Mwashiuya.
Comments
Post a Comment