KWA UFUPI MFAHAMU DIBLO DIBALA 'MASHINE GUN' GWIJI WA KUTEKENYA NYUZI ZA GITAA
Diblo Dibala |
Akiwa na umri wa miaka 15, alishinda mashindano ya kusaka vipaji ambapo kutokana na umahiri wake wa kucharaza gitaa ulimfanya ajiunge na bendi ya marehemu Franco, TPOK Jazz
Hata hivyo alikaa na kundi hilo kwa muda mfupi na baadae akaenda kushirikiana na makundi ya Vox Afrika, Orchestra Bella Mambo na Bella Bella ambapo bendi yake ya kwanza ilikuwa ya Kanda Bongo Man
Mwaka 1979 alihamia Ubelgiji kabla ya mwaka kujiunga na bendi ya Kanda Bongo Man mjini Paris Ufaransa amabapo alifyatua albamu yake ya kwanza mwaka huo na kuipa jina la Lyole
Tangu kipindi hicho Diblo alizidi kupanda chati hasa baada ya kufanya kazi na wanamuziki kama Pepe Kale na makundi mengine mengi yaliyokuwa yakipiga muziki wa Soukous
Mwaka 1980 aliamua kuunda bendi yake aliyoipa jina la Loketo ambapo alikuwa akishirikiana na mwanamuziki Aurlus Mabele , hata hivyo miaka michache baadaye bendi hiyo ilivunjika hali ambayo ilimlazimu mwaka 1990 kuunda kundi jipya alilolipa jina la Matchatcha, ambalo hadi sasa linaendelea kufanya kazi baada ya kulifanyia marekebisho mbalimbali.
Comments
Post a Comment