LUBUVA APATA MRITHI KWENYE TUME YA UCHAGUZI YA TAIFA
Jaji wa mahakama ya Rufaa Mh. Semistocles Kaijage akizungumza na vyombo vya habari mara baada ya kuapishwa kuwa jaji ilikuwa mwaka 2012 |
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli, leo tarehe 22 Desemba, 2016 amemteua Jaji wa Mahakama ya Rufaa, Mhe. Jaji Semistocles Kaijage kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC).
Taarifa
iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi imeeleza kuwa
Mhe. Jaji Semistocles Kaijage ameteuliwa kuongoza Tume hiyo kwa kipindi
cha miaka 5 kuanzia tarehe 20 Desemba, 2016.
Mhe. Jaji Semistocles Kaijage anachukua nafasi ya Mhe. Jaji Mstaafu Damiani Lubuva ambae muda wake wa kuwa Mwenyekiti umemalizika rasmi mnamo tarehe 19 Desemba, 2016.
Aidha, Mhe. Rais Magufuli amemteua Mhe. Jaji Mstaafu Hamid Mahamoud Hamid kuwa Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kwa kipindi kingine cha miaka 5 kuanzia tarehe 20 Desemba, 2016.
Mhe. Jaji Mstaafu Hamid Mahamoud Hamid alikuwa Makamu Mwenyekiti wa NEC na amemaliza kipindi chake cha kwanza cha miaka 5 mnamo tarehe 19 Desemba, 2016.
Halikadhalika, Mhe. Rais Magufuli pia amemteua Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufaa, Mhe. Jaji Harold Reginald Nsekela kuwa Kamishna wa Maadili katika Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma kwa kipindi cha miaka 5 kuanzia tarehe 20 Desemba, 2016.
Mhe. Jaji Mstaafu Nsekela anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Mhe. Jaji Mstaafu Salome S. Kaganda ambae amestaafu mnamo tarehe 10 Desemba, 2016.
Katika hatua nyingine, Mhe. Rais Magufuli amewateua Majaji 4 wa Mahakama Kuu kuwa Majaji wa Mahakama ya Rufani kuanzia leo tarehe 22 Desemba, 2016 kama ifuatavyo:-

- Mhe. Jaji Dkt. Gerald Ndika
- Mhe. Jaji Jackobs Mwambegele
- Mhe. Jaji Rehema Kiwanga Mkuye
- Mhe. Jaji Sivangilwe Sikalalilwa Mwangesi
Comments
Post a Comment