LUKUVI APOKONYA MASHAMBA 21 YASIYOENDELEZWA

Waziri wa ardhi, nyumba na maendeleo ya makazi
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. William Lukuvi, amesema hadi sasa ameshagawa kwa wananchi mashamba 21 ambayo yalikuwa hajaendelezwa huku wamiliki wa mashamba mengine zaidi ya 5,000 wakiwa wameshaandikiwa barua ya kutoa maelezo ya kwanini hawajaendeleza mashamba yao.
Akizungumza na EATV Mhe. Lukuvi amesema hatua hiyo ni moja kati ya hatua zitakazosaidia kumaliza migogoro ya ardhi, katika maeneo mengi ya nchi huku akiwahakikishia watanzania kuwa ndani ya miaka mitano tatizo la hilo litakuwa limekwisha kabisa.
Wakati huo huo Mhe. Lukuvi amesema kuanzia mwezi wa saba mwaka 2017 wataweka mfumo onganisha wa taarifa zote za ardhi kwa kutumia hati za kidigitali badala ya zile za karatasi na tayari wamempata mtengenezaji wa mfumo huo na kazi ya ubadilishaji kwa mwananchi mmoja mmoja imeanza kwa kurekebisha nyaraka mbalimbali ili zoezi litakapoanza kusiwe na vikwazo.

Comments